Mamlaka ya ushindani wa kibiashara nchini imeidhinisha ununuzi wa asilimia 51 ya hisa za kampuni ya bina ya Monarch na kampuni tatu ambazo ni Ondoba Limited, Kenyoro Limited na Equico Thirteen Limited bila masharti yoyote.
Kampuni ya Ondoba ni kampuni mpya iliyoasisiwa kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya fedha. Kenyoro Limited nayo ni kampuni iliyosajiliwa nchini ambayo huwekeza katika sekta ya fedha sawa na Equico Thirteen Limited.
Kampuni ya bima ya Monarch Insurance Company Limited ambayo inauza hisa ni kampuni iliyosajiliwa nchini kwa ajili ya kutoa bima ya jumla, ya magari na hata ya maisha.
Kulingana na wahusika, sababu kuu ya uuzaji na ununuzi huo wa hisa kukuza biashara na kuipanua kupitia kuboresha mipango na kutekeleza mkakati uliojikita katika ushirkiano na wanahisa hao wapya.