Home Biashara UNDP na Benki ya Dunia zapiga jeki uwekezaji Kenya

UNDP na Benki ya Dunia zapiga jeki uwekezaji Kenya

0

Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, UNDP, Benki ya Dunia na Mamlaka ya Uwekezaji Nchini, KenInvest leo Ijumaa zimetangaza ushirikiano mpya unaokusudia kuendeleza na kutekeleza Mpangokazi wa Kuwezesha Uwekezaji na Mkakati wa Kuvutia Uwekezaji wa Kigeni wa Moja kwa Moja, FDI. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Waziri wa Biashara Rebecca Miano aliupongeza akisema utafanya iwe rahisi kwa wawekezaji kuwekeza, kufanya biashara na kupanua shughuli zao humu nchini.

Kupitia ushirikiano huo, Waziri Miano alisema Kenya italainisha michakato inayohusiana na uvutiaji wa uwekezaji wa humu nchini na kigeni na pia kusaidia kuimarisha uratibu na ushirikiano miongoni mwa wadau katika nyanja ya uwekezaji.

Waziri aidha alipongeza wajibu unaotekelezwa na Baraza la Kitaifa la Uwekezaji ambalo limejukumiwa kutoa mkakati wa uratibu ili kuunga mkono ukuaji wa uwekezaji nchini Kenya.

“Tumeweka lengo kama nchi la kuvutia Uwekezaji wa Kigeni wa Moja kwa Moja wa hadi dola bilioni 10 za Marekani,” alisema Waziri Miano.

Kupitia ushirikiano huo, serikali itatumia mtandao wa UNDP duniani kutekeleza Mpangokazi wa Kuwezesha Uwekezaji humu nchini.

 

 

Website | + posts