Home Kimataifa Umeme waanza kurejea Nigeria kufuatia giza totoro

Umeme waanza kurejea Nigeria kufuatia giza totoro

Umeme umekuwa ukitoweka mara kwa mara nchini Nigeria na kisa cha hivi punde kaunzia mapema Alhamisi iliathiri majimbo yote 36 na mji mkuu Abuja kabla ya kurejeshwa katika maeneo kadhaa.

0

Umeme umeanza kurejeshwa nchini Nigeria baada ya taifa zima kutumbukia katika giza totoro kufuatia kutoweka kwa umeme kwa zaidi ya saa kumi kutokana na moto uliozuka na kutatiza usambazaji umeme.

Umeme umekuwa ukipotea mara kwa mara nchini Nigeria na kisa cha hivi punde kuanzia mapema jana Alhamisi kiliathiri majimbo yote 36 na mji mkuu wa Abuja, kabla ya kurejeshwa katika maeneo kadhaa.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ameahidi kuimarisha usambazaji wa umeme kwa kuruhusu mashirika ya serikali kuunda mitambo yao ya kusambaza umeme.

Website | + posts