Ndoto ya Tanzania almaarufu Taifa Stars kusajili ushindi wa kwanza katika historia ya kombe la AFCON imezimwa baada ya kulazimishwa kwenda sare ya 1-1 na Zambia.
Mechi hiyo ya kundi F ilipigwa jana Jumapili jioni mjini San Pedro nchini Ivory Coast.
Tanzania walichukua uongozi katika dakika ya 11 kupitia kwa Simon Musuva.
Taifa Stars walipigwa jeki baada ya Rodrick Kabwe kulishwa kadi ya pili ya njano na kufurushwa uwanjanj mwishoni mwa kipindi cha kwnaza.
Zambia ukipenda Chipolopolo walijizatiti kipindi cha pili naye Patson Daka akakomboa bao hilo kunako dakika ya 88.
Tanzania watakumbana na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC Jumatano katika mechi ya mwisho huku Morocco wakifunga kazi na Zambia.
Morocco wanaongoza kundi F kwa pointi 4 wakifuatwa na DRC kwa alama 2 sawa na Zambia nao Tanzania wana pointi 1.