Home Kimataifa Ukraine haina uhusiano wowote na ajali ya ndege – Zelensky

Ukraine haina uhusiano wowote na ajali ya ndege – Zelensky

0
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

Ukraine haikuhusika katika kifo kilichoripotiwa cha bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin, Rais Volodymyr Zelensky anasema.

“Hatuhusiki katika hali hii, hiyo ni hakika. Nadhani kila mtu anafahamu ni nani anayehusika,” Zelensky aliwaambia waandishi wa habari huko Kyiv.

Zelensky alifanya mzaha kuhusu wito wa Ukraine kwa mataifa mengine kwa ajili ya ndege zaidi za kupambana na uvamizi wa Urusi.

“Ukrainia ilipotoa wito kwa nchi za ulimwenguni kuhusu ndege, hatukumaanisha hivi,” anasema. “Lakini hii kwa njia fulani hakika itasaidia,” anaongeza.

Alisisitiza juu ya Kyiv kuwa na uhusiano wowote na kifo kilichoripotiwa cha Prigozhin.