Home Michezo Uingereza wahemeshwa na Nigeria kabla ya kutinga robo fainali ya Kombe la...

Uingereza wahemeshwa na Nigeria kabla ya kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia

0

Uingereza almaarufu Three Lionesses wamekabiliwa na wakati mgumu dhidi ya Nigeri Superr Falcons kabla ya kuwashinda kupitia matuta ya penalti na kujikatia tiketi kwa robo fainali ya Kombe la Dunia kwa akina dada mjini Brisbane nchini Australia.

Timu hizo zilitoka sare tasa baada ya dakika 90 kabla ya Uingereza ambao ni mabingwa wa Ulaya kushinda penalti 4 -2 na kutinga hatua ya nane bora.

Lauren James alipigwa kadi nyekundu kwa kumkanyaga mchezaji  wa Nigeria Michelle Alozzie mwishoni mwa mechi.

Uingereza watachuana na mshindi kati ya Jamaica na Colombia katika hatua ya kwota fainali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here