Home Habari Kuu Uhuru, Mama Ngina wamsifu mpiganiaji uhuru Muthoni wa Kirima

Uhuru, Mama Ngina wamsifu mpiganiaji uhuru Muthoni wa Kirima

Muthoni wa Kirima alifariki tarehe nne mwezi Septemba akiwa na umri wa miaka 92.

0

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Mama taifa Ngina Kenyatta, wameungana na wakenya katika kusherehekea maisha ya aliyekuwa mpiganiaji uhuru Muthoni Kirima.

Uhuru alimtaja Muthoni wa Kirima, kuwa mzalendo na mmoja wa mashujaa wa Mau Mau waliopigania uhuru wa taifa hili.

Rais huyo mstaafu alisema nyayo za Muthoni zilitekeleza wajibu mkubwa katika kuunga mkono viongozi wengine waliokuwa na mawazo sawa katika vita dhidi ya ukoloni na ukuaji wa kijamii na kiuchumi hapa nchini.

“Atasalia kuwa kata historia ya taifa hili katika vita dhidi ya ukoloni. Atakumbukwa sio tu kwa ujasiri wake, lakini pia kwa bidii yake,” alisema Uhuru.

Katika rambirambi yake, Mama Ngina alisema kifo cha Muthoni kimeacha pengo kubwa ambalo itakuwa vigumu kuliziba, huku akipongeza kujitolea kwake katika kupigania uhuru wa taifa hili.

“Nafurahia kumbukumbu ambazo sisi na Muthoni wa Kirima pamoja na wengine tulikuwa nazo. Namshukuru Mungu kwa fursa na heshima ya kumjua na kushiriki naye katika kipindi kilichokuwa na changamoto hapa nchini, pamoja na wengine wengi,” alisema mama Ngina.

Muthoni wa Kirima alifariki tarehe nne mwezi Septemba akiwa na umri wa miaka 92.

Website | + posts