Home EURO 2024 Uhispania yatinga awamu ya 16 bora kombe la Euro

Uhispania yatinga awamu ya 16 bora kombe la Euro

0
kra

Timu ya Uhispania wamejiunga na wenyeji Ujerumani kwenye awamu ya pili ya kipute cha bara Ulaya, baada ya ushindi mwembamba wa bao moja dhidi ya Italia ugani Veltins Alhamisi usiku.

Bao hilo la pekee lilikuwa la kujifunga kutoka kwa beki Riccardo Calafiori dakika ya 55.

kra

Ushindi huo,unaiweka Uhispania uongozini pa kundi B kwa alama sita, ikifuatwa na ltalia kwa alama tatu, huku na Albania zikiwq na pointi moja kila moja.

Katika matokeo ya mechi za kundi C, Uingereza na Denmark zilitoka sare ya bao moja kwa moja uwanjani Deutsche Bank Park.

Harry Kane alitangulia dakika ya 18 kisha Morten Hjulmand akakomboa kwa Denmark dakika ya 34.

Slovenia na Serbia walitoka pia sare iyo hiyo ugani Allianz,Žan Karničnik akipachika bao dakika ya 69 nayo Serbia ikasawazisha dakika ya tano ya muda wa majeruhi kupitia kwa Luka Jović.

Ijumaa ni zamu ya Slovakia na Ukraine kumemenyana saa kumi jioni katika kundi E, Poland dhidi ya Austria saa moja kundini C, kisha Uholanzi wafunge ratiba dhidi ya Ufaransa saa nne usiku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here