Home Michezo Uhispania waikwatua Italia na kutinga fainali ya UEFA Nations League

Uhispania waikwatua Italia na kutinga fainali ya UEFA Nations League

Uhispania watashuka mjini Roterderm Jumapili hii kwa fainali dhidi ya Croatia.

0

Bao la dakika za mwisho mwisho lake Joselu, liliwapa Uhispania ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya mabingwa wa Ulaya Italia, na kufuzu kwa fainali ya kombe la UEFA Nations League katika nusu fainali ya pili iliyopigwa Alhamisi usiku mjini Enschede Ubolanzi.

Yeremy Pino aliwaweka Hispania uongozini baada ya kumpokonya mpira beki mkongwe Leonardo Bonucci.

Ciro Immobile aliisawazishia Italia kupitia penati, baada ya limbukeni Robin le Normand kuunawa mpira.

Uhispania watashuka mjini Roterderm Jumapili hii kwa fainali dhidi ya Croatia.

Wekundu wa Uhispania watakuwa wakipiga fainali hiyo kwa mara ya pili baada ya kuduwazwa na Ufaransa mwaka 2021.

Awali Jumapili Uholanzi itakumbana na Italia katika mkwangurano wa kuwania nafasinya tatu.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here