Home EURO 2024 Uhispania, Uswizi na Italia wavuna ushindi

Uhispania, Uswizi na Italia wavuna ushindi

0
kra

Kipute cha mataifa bingwa ya bara Europa kinachoendelea nchini Ujerumani, kiliingia siku ya pili hapo jana na kuandikisha matokeo mseto. Katika mchuano wa kwanza, Uswizi iliilaza Hungary magoli matatu kwa moja ugani RheinEnergieStadio.

Kwadwo Duah alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 12 naye cMichel Aebischer akaongeza la pili dakika ya 45.Katika kipindi cha pili, Hungary walijizatiti na kupachika bao dakika ya 66 kupitia mshambulizi Barnabás Varga.

kra

Hata hivyo, nguvu mpya Breel Embolo aliipa Uswizi la tatu katika dakika za majeruhi(90+3) na kufanya mambo kuishia magoli matatu kwa moja.

Baadaye, Uhispania na Croatia walijitosa ugani huku kila timu ikijivunia wachezaji Nyota kama vile Rodri, Morata na Carvajal kwa upande wa Uhispania na Modric, Perisich na Kovacic kwa upande wa Croatia.

Mchuano ulianza kwa kasi na ilipofika dakika ya 29, mshambulizi matata Álvaro Morata aliiweka Uhispania uongozini kabla ya Winga Fabián Ruiz kuongeza la pili dakika mbili baadae.

Dani Carvajal alifunga la tatu na la mwisho la mchuano huo katika dakika za mazidadi (45+2).Kwenye kipindi cha pili, Croatia walizawadiwa mkwaju wa adhabu ila ulipanguliwa na mlinda lango.

Croatia waliufwata mpira huo na kufunga ila bao hilo likakataliwa hivyo kufanya mambo kuishia magoli matatu kwa sufuri.

Saa nne usiku ilikuwa zamu ya Italia ( Gli Azzurri) na Albania (Wekundu na Weusi). Albania walipata bao dakika ya kwanza kupitia Nedim Bajrami baada ya Italia kufanya masihara karibu na lango.

Hata hivyo, Italia walijibu dakika ya 11 pale Alessandro Bastoni aliandaliwa mpira wa kona na kufunga kwa kichwa.Dakika tano baadaye Nicolò Barella alivurumusha kwajo nzito lililomwacha hoi mlinda lango Thomas Strakosha.

Mambo yalisalia vile hadi mchuano huo ulipotamatika.

Leo itakuwa fursa ya Poland dhidi ya Uholanzi saa kumi jioni, Slovenia wakabane na Denmark saa moja kisha Serbia wamalize na Uingereza sa nne usiku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here