Home Michezo Uhispania kumenyana na Uingereza fainali ya Kombe la Dunia kwa wanawake

Uhispania kumenyana na Uingereza fainali ya Kombe la Dunia kwa wanawake

0
SYDNEY, AUSTRALIA - AUGUST 16: Georgia Stanway (C) and England players celebrate after the team's 3-1 victory and advance to the final following the FIFA Women's World Cup Australia & New Zealand 2023 Semi Final match between Australia and England at Stadium Australia on August 16, 2023 in Sydney, Australia. (Photo by Catherine Ivill/Getty Images)

Uingereza itapambana dhidi ya Uhispania kwenye fainali ya makala ya 9 ya fainali za kombe la dunia kwa wanawake.

Uingereza imefuzu kwa fainali Jumatano baada ya kuwadhalilisha wenyeji Australia maarufu kama Matildas walipowazabua magoli 3-1,katika nusu fainali ya mwisho  iliyopigwa uwanjani Olympic mjini Sydney Australia.

Ella Ann Toone aliwaweka Uingereza kifua mbele kwa goli la dakika ya 36 kabla ya Samantha Kerr, kuwarejesha mchezoni wenyeji katika dakika ya 63 naye Lauren Hemp kupachika bao la pili kwa Three Lionesses dakika 7 baadaye.

Alessia Russo alikomelea msumari wa mwisho kwa jeneza la Australia kunako dakika ya 86 na kuhakikisha Uingereza watacheza fainali siku ya Jumapili Agosti 20.

Uhispania walikuwa wa kwanza kufuzu kwa fainali siku ya Jumatano kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uswidi katika nusu fainali.

Uingereza na Uhispania watakuwa wakicheza fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here