Home Kimataifa Uhesabu watu nchini Burundi waingia wiki ya tatu

Uhesabu watu nchini Burundi waingia wiki ya tatu

0
kra

Shughuli ya kuhesabu watu nchini Burundi imeingia wiki ya tatu katika zoezi litakalokamilika Septemba 15.

Taifa hilo la Afrika Mashariki linaheabu raia wake kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008, ikiwa mara ya tatu kwa zoezi hilo baada ya mwaka 1962 na 1990 .

kra

Hata hivyo makarani wa kuhesabu watu wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kukosa watu katika majumba wanapozuru kuwahesabu,kucheleweshwa kupokea malipo na changamoto ya usafiri, wengi wakilazimika kutembea kwa mwendo mrefu.

Serikali ya Burundi imetenga dola za Kiamrekani milioni 22.85, nayo benki ya Dunia ikiahidi kuongezea milioni 6.5 kwa mchakato huo.

Burundi imegawanyika kwa mikoa mitano ya Gitega,Bujumbura, ,Butanyera, Buhumuza na Burunga.

Website | + posts