Home Habari Kuu Ugonjwa wa kipindupindu wazuka kaunti ya Garissa

Ugonjwa wa kipindupindu wazuka kaunti ya Garissa

Mkurugenzi wa afya wa kaunti hiyo Adan Hussein, alisema kisa cha kwanza kiligunduliwa tarehe tisa mwezi huu wa Oktoba.

0
Ugonjwa wa kipindupindu wazuka Garissa.

Visa vipya vya ugonjwa wa kipindupindu, vimeripotiwa katika kambi ya wakimbizinya Dadaa, kaunti ya Garissa.

Kulingana na idara ya afya ya kaunti hiyo, visa sita vya ugonjwa huo, viliripotiwa katika kambi ya wakimbizi ya Hagdera.

Mkurugenzi wa afya wa kaunti hiyo Adan Hussein, alisema kisa cha kwanza kiligunduliwa tarehe tisa mwezi huu wa Oktoba.

“Tunakabiliwa na wimbi la pili la maambukizi ya kipindupindu, lakini tunakabiliana na hali hiyo Kwa kuweka vituo vya dharura pamoja na kusambaza vifaa vinavyohitajika vya matibabu,” alisema Hussein.

Serikali ya kaunti ya Garissa tayari imetuma wahudumu wa afya ya jamii katika kambi hiyo ya wakimbizi, ili kuhamasisha umma kuhusiana na ugonjwa huo.

“Tunafuatilia kwa karibu hali ilivyo Hagadera kwa lengo la kukabiliana na maambukizi hayo,” aliongeza Hussein.