Home Biashara Ugavi wa mapato ya mbuga za wanyapori na serikali za kaunti wasifiwa

Ugavi wa mapato ya mbuga za wanyapori na serikali za kaunti wasifiwa

kra

Muungano wa wataalamu wa uhifadhi wa wanyamapori, umelipokea vyema agizo la Rais William Ruto, kuhusiana na ugavi wa mapato yanayotoka kwenye mbuga za wanyamapori linaloruhusu Kaunti husika kupata mgao wa asilimia 50 ya mapato hayo.

Daktari Jirmo Tuqa, ambaye ni katibu wa muungano huo, alitoa wito kwa serikali kuweka mikakati ya mfumo thabiti wa usimamizi wa fedha, utaratibu wa ukaguzi pamoja na kuanzishwa kwa taasisi ya uwazi, ili kuyasimamia mapato hayo.

kra

Dakta Jirmo, alisema jamii zinazoishi maeneo yaliyo na idadi kubwa ya wanyamapori zitafaidika mno na mapato hayo.

Dakta Jirmo alisema licha ya manufaa ya wanyamapori, idadi yao imepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na miongoni mwa matatizo mengine, uvamizi wa makazi yao, sawa na kufungwa kwa njia zao za kuhama.

feedback@kbc.co.ke | Website | + posts
Website | + posts