Home Michezo Uganda yatwaa mataji ya soka katika michezo ya shule za upili Afrika...

Uganda yatwaa mataji ya soka katika michezo ya shule za upili Afrika Mashariki nchini Rwanda

Wiyeta Girls kutoka kenya ilinyakua nishani ya fedha baada ya kushindwa mabao mawili kwa nunge na Kawempe Muslim kutoka Uganda kwenye fainali.

0

St Mary’s Boarding School Kitende na Kawempe Muslim kutoka Uganda ndio mabingwa wa soka kwa wavulana na wasichana mtawalia, katika makala ya mwaka huu ya 20 ya  michezo ya shule za sekondari Afrika Mashariki, yaliyokamilika Jumapili mjini Huye nchini Rwanda.

Kitende walinyakua taji ya soka ya wavulana kwa mara ya 15 baada ya kuwabwaga wenzao kutoka Uganda Amus College mabap 4-2 kupitia mikiki ya penalti kufuatia sare ya bao 1 katika muda wa dakika 90.

Shule ya upili ya Kibuli pia ya Uganda ilinyakua nishani ya shaba baada ya kuwalemea wenzao St. Henry’s College Kitovu mabao 2-1 katika pambano la kuwania nafasi ya tatu na nne.

Wiyeta Girls Kitale wakicheza fainali dhidi ya Kawempe Muslim

Wiyeta Girls kutoka Kenya ilinyakua nishani ya fedha baada ya kushindwa mabao mawili kwa nunge na Kawempe Muslim kutoka Uganda kwenye fainali.

Nyamira Girls ya Kenya ilitwaa ubingwa wa magongo huku Kwanthanze wakihifadhi taji ya voliboli kwa wasichana wakati Koyonzo Boys ya Kenya wakinyakua taji ya raga kwa wachezaji 15 upande.

Koyonzo Boys mabingwa wa Raga ya wachezaji saba
Nyamira Girls mabingwa wa magongo
Kwanthanze mabingwa wa Voliboli