Uganda hatimaye imefungua mradi wa kuzalisjha umeme Karuma ambao umekuwa ukikarabatiwa kwa miaka 11 iliyopita.
Mradi huo ulianza kujengwa Disemba mwaka 2013 kwa gharama ya shilingi bilioni 213 za Kenya au dola Bilioni 1.688,huku shilingi bilioni 177 zikiwa mkopo kutoka benki ya Exim ya China wakai kiwango kilichosalia kikitolewa na serikali ya Uganda..
Mradi wa Karuma unazalisha kawi ya megawati 600 na kufikisha kiwango cha megawati 2,000 ambazo zimekuwa zikizalishwa kutokana na maji.
Rais Yoweri Museveni alifungua mradi huo wa umeme.