Home Habari Kuu Ugaidi ungali tishio kwa Kenya, asema Waziri Kindiki

Ugaidi ungali tishio kwa Kenya, asema Waziri Kindiki

0

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Prof. Kithure Kindiki ametaja ugaidi kuwa miongoni mwa matishio makuu zaidi yanayoikabili Kenya. 

Anasema serikali imeazimiia kutumia njia mbalimbali kukabiliana na watu wanaotishia amani na usalama wa nchi hiyo.

“Shambulio la bomu lililotekelezwa kwenye Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi Agosti, 1998 lilichochea kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali kukabiliana na tishio la ugaidi,” alisema Prof. Kindiki alipofika mbele ya kamati ya bunge inayoangazia malipo ya fidia kwa Wakenya walioathiriwa na shambulizi hilo.

“Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa vikosi maalum kama vile Kikosi cha Polisi wa Kupambana na Ugaidi, ATPU, Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi, NCTC, Jopokazi la Pamoja la Ugaidi, JTFF, Kituo cha Kuripoti Masuala ya Fedha, FRC, Kikosi cha Walinzi wa Pwani wa Kenya, Kitengo cha Uhalifu Ulioratibiwa Unaohusisha Nchi Kadhaa, TOCU na Mamlaka ya Urejeshaji wa Mali, ARA

Waziri Kindiki aliongeza kuwa sheria muhimu zimepitishwa kukabiliana na ugaidi ikiwa ni pamoja na Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya Mwaka 2012.

 

Website | + posts