Home Taifa Ufisadi utawaramba, Ruto awaonya Mawaziri wapya

Ufisadi utawaramba, Ruto awaonya Mawaziri wapya

0
kra

Rais William Ruto ametoa onyo kali kwa mawaziri wapya na Makatibu wao akiwataka kutojihusisha katika visa vya ufisadi la sivyo wakione cha mtema kuni.

Ruto ameapa kufanya kila awezalo kuimarisha vita dhidi ya zimwi la ufisadi nchini.

kra

Ametoa onyo hilo mapema leo Jumatatu aliposhiriki kikao na Mawaziri hao pamoja na makatibu wao katika Ikulu ya Nairobi.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Wakati wa mkutano huo, Rais Ruto aliwataka mawaziri hao na makatibu wao kutoa kipaumbele kwa mipango bora na ambayo itasaidia kubuni nafasi za ajira kwa vijana humu nchini.

“Utendakazi wenu unapaswa kuendana na kiapo mlichokula,” kiongozi wa nchi aliwaambia mawaziri hao walioapishwa wiki jana.