Ufaransa wametwaa dhahabu ya kwanza ya Olimpiki baada ya kuwalemea mabingwa mara bili Fiji pointi 28-7 katika fainali ya raga wachezaji saba.
Matokeo hayo yalizima ndoto ya Fiji kunyakua dhahabu ya tatu mtawali katika michezo ya Olimpiki, baada ya kutawazwa mabingwa mwaka 2016 na 2020.
Wenyeji Ufaransa wamenyakua dhahabu 1 fedha 2 na shaba 1.
Afrika Kusini imenyakua nishani shaba baada ya kuikung’uta Australia pointi 26-19.