Home Michezo UEFA yaahirisha mechi zote zilizoratibiwa kuchezwa Israel kwa wiki mbili

UEFA yaahirisha mechi zote zilizoratibiwa kuchezwa Israel kwa wiki mbili

0

Shirikisho la Kandanda barani Ulaya, UEFA limeamua kuahirisha mechi zote zilizoratibiwa kuandaliwa nchini Isreal kwa majuma mawili yajayo kutokana na makabiliano yanayoendelea katika ukanda wa Gaza.

Israel ilitangaza vita dhidi ya kundi la Hamas jana Jumapili kufuatia mashambulizi ya kundi hilo la wanamgambo yaliyosababisha kuawa kwa mamia ya raia wake.

Baadhi ya mechi zilizoathiriwa ni mchuano kati ya Israel na Uswizi uliokuwa upigwe Oktoba 10, huku ile ya Oktoba 15 baina ya Israel na Kosovo ikitegemea na hali itakavyokuwa.

Website | + posts