Home Habari Kuu UDA kufanya uchaguzi wa mashinani Ijumaa

UDA kufanya uchaguzi wa mashinani Ijumaa

0

Chama tawala cha United Democratic Alliance,UDA kinaandaa uchaguzi wake wa mashinani siku ya Ijumaa ,April 26 .

Kwa mjibu wa msimamizi wa bodi ya uchaguzi Anthony Mwaura vituo vya kupiga kura vitafunguliwa saa tatu asubuhi na kufungwa saa tisa alasiri.

Kaunti zitakazoshiriki zoezi hilo ni Nairobi, Busia, Narok, West Pokot na  Homa Bay.

Katika kaunti ya Nairobi yenye wanachama 853,000, kivumbi kinatarajiwa katika wadhifa wa mwenyekiti unaowaniwa na Gavana Johnson Sakaja na Mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya.

Chama hicho pia kimetenga ndege mbili za helikopta ili kusafirisha vifaa vya kupigia kura katika maeneo yaliyoathirika vibaya na mafuriko.

Uchaguzi wa mashinani baadaye utapisha uchaguzi wa kitaifa .