Home Habari Kuu UDA kuandaa mkutano wa Baraza la Kitaifa la Uongozi Ijumaa

UDA kuandaa mkutano wa Baraza la Kitaifa la Uongozi Ijumaa

0

Chama cha United Democratic Alliance, UDA kinachoongozwa na Rais William Ruto kitaandaa mkutano wa Baraza la Uongozi wa chama hicho leo Ijumaa katika ukumbi wa Bomas.

Kulingana na arifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Cleophas Malala, kikao hicho kitaongozwa na Rais Ruto.

Yamkini manaibu wenyekiti wawili watatangazwa katika kikao hicho.

Mkutano huo unatarajiwa kuziba nyufa na kuzima minong’ono ambayo imekuwa chamani, na kuweka mikakati ya uchaguzi mkuu wa chama unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu.

Website | + posts