Home Kimataifa Uchaguzi Zimbabwe: Mnangagwa kuendelea kuongoza

Uchaguzi Zimbabwe: Mnangagwa kuendelea kuongoza

0

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ataendelea kuongoza taifa hilo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Hii ni baada ya tume ya uchaguzi nchini humo Zimbabwe Electoral Commission – ZEC, kumtangaza kuwa mshindi kwenye uchaguzi wa urais Jumamosi jioni.

Mnangagwa wa chama cha Zanu PF na ambaye ana umri wa miaka 80 alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 52 ya kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake Nelson Chamisa, wa umri wa miaka 45,wa chama cha Citizens Coalition for Change akipata asilimia 44 ya kura zote zilizopigwa.

Raia wa taifa la Zimbabwe walipiga kura kwenye uchaguzi mkuu Jumatano Agosti 23, 2023, lakini muda wa uchaguzi ukaongezwa kwa siku nyingine moja baada ya tume ya uchaguzi kukosa kuwasilisha karatasi za kupigia kura katika mji mkuu Harare na Bulawayo.

Majibu hayo ya uchaguzi huenda yakawa ya kuvunja moyo kwa raia wengi wa Zimbabwe ambao walitumai kwamba Chamisa ataibuka mshindi ili kuokoa nchi hiyo kutokana na matatizo ya kiuchumi. Uchumi wa nchi hiyo umekuwa ukizorota kwa miaka mingi sasa kutokana na kile kinachotajwa kuwa usimamizi mbaya wa nchi.

Mnangagwa aliingia uongozini baada ya mtangulizi wake Robert Mgabe kuondolewa kupitia mapinduzi Novemba 2017. Kipindi chake cha kwanza uongozini kilianza rasmi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2018 ingawa majibu ya uchaguzi huo yalikumbwa na mzozo.

Website | + posts