Home Kimataifa Uchaguzi wa chama cha wanaosomea udaktari wafutiliwa mbali

Uchaguzi wa chama cha wanaosomea udaktari wafutiliwa mbali

0
kra

Serikali imetupilia mbali uchaguzi wa viongozi wa chama cha wanafunzi wa kozi za udaktari nchini almaarufu Medical Students’ Association of Kenya -MSAKE.

Hatua hiyo ilichochewa na kile kinachoripotiwa kuwa ukiukaji wa katiba ya chama hicho.

kra

Wakili wa serikali katika afisi ya usajili wa vyama nchini Felix Mukuvi, alitupilia mbali majibu ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 27, 2023.

Kulingana naye, kifungu nambari saba cha katiba ya chama hicho kilikiukwa na kwamba wawili kati ya waliochaguliwa ambao ni Andrew Were na John Kibet, sio wanafunzi wa udaktari.

Afisi hiyo ya usajili wa vyama imeshauri wafadhili pamoja na umma kutafuta maelekezo kutoka kwayo kabla ya kujihusisha na viongozi ambao uchaguzi wao umebatilishwa.

Baada ya uchunguzi wa muda, afisi ya usajili wa vyama ilisema kwamba katiba ya chama cha madaktari wanafunzi ilikiukwa kwani Were na Kibet hawakuhitimu kuwania wadhifa wowote.

Mukuvi alisema kwamba waraka waliopokea kutoka kwa katibu mkuu wa chama hicho cha wanafunzi wa udaktari unaelezea kwamba Were na Kibet walikuwa wanafunzi awali lakini walishakamilisha masomo.

Website | + posts