Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa onyo kuhusu uwezekano wa kutekelezwa kwa shambulizi la kigaidi kwa raia wake nchini humo.
Kwenye taarifa iliyotolea leo Ijumaa, ubalozi huo umeonya kuhusu uwezekano wa shambulizi dhidi ya raia wake na raia wengine wa kigeni katika maeneo yanayotembelewa na watalii kwa wingi katika kaunti ya Nairobi na maeneo mengine nchini Kenya.
Maeneo yanayolengwa ni kama vile mikahawa, maeneo ya kuuza vyakula, balozi, supamaketi na masoko.
Pia taarifa hiyo imeonya juu ya uwezekano wa mashambulizi katika shule, vituo vya polisi, maeneo ya kuabudu na maeneo mengine ambayo ushuhudia idadi kubwa ya watalii.
Ubalozi wa Marekani umewataka watu kutahadhari na misongamano na maeneo yaliyo na watu wengi.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikutoa sababu iliyochangia kupangwa kwa shambulizi hilo.