Home Kimataifa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania wasitisha huduma kisa tatizo la Internet

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania wasitisha huduma kisa tatizo la Internet

0
kiico

Taifa jirani la Tanzania lilikumbwa na tatizo la kukatika kwa mtandao wa Internet jana Jumapili Mei 12, 2024 kuanzia saa tano asubuhi.

Waziri wa Mawasiliano nchini humo Nape Nnauye alitangaza kwamba kampuni ambazo zinatoa huduma za nyaya za baharini ziliarifu kuhusu hitilafu kwenye nyaya zao iliyosababisha kukatika kwa huduma za Internet nchini humo.

Nape alitaja kampuni za Seacom na EASSy, akisema ndizo zilitaarifu kuhusu hitilafu hiyo.

Maelezo ya kampuni hizo mbili yalisema kwamba huduma zilizoathirika ni kati ya Msumbiji na eneo la Afrika Kusini.

Waziri Nape hata hivyo alisema kwamba jitihada za kutatua tatizo hilo zilikuwa zinaendelea, akiongeza kwamba huduma za Internet zingekuwa kwa kiwango cha chini.

Tatizo hilo lilisababisha ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kutangaza kwamba haungepokea wageni na hivyo kusitisha kwa muda miadi yote ya leo Jumatatu Mei 13, 2024.

Taarifa ya Ubalozi huo ilisema kwamba ratiba nyingine itapangwa ya kupokea na kuhudumia wageni walioathirika lakini walio na dharura watapata huduma leo.

kiico