Home Burudani UB40 kutumbuiza nchini Uganda Disemba 2023

UB40 kutumbuiza nchini Uganda Disemba 2023

0

Kampuni ya maandalizi ya tamasha nchini Uganda iitwayo Talent Africa Group imetangaza ujio wa kundi la muziki la UB40 nchini humo Disemba, 2023.

Katika kikao na wanahabari huko Naguru jijini Kampala nchini Uganda, wawakilishi wa kampuni hiyo walitangaza kwamba kundi hilo la muziki kutoka Uingereza litaandaa tamasha katika uwanja wa Kololo Independence, Disemba 21, 2023.

Kundi hilo lilifanya tamasha kwa mara ya kwanza nchini Uganda mwaka 2008 katika uwanja wa Lugogo jijini Kampala, tamasha ambayo ilihudhuriwa na watu wapatao elfu 30.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Talent Africa Group Ali Alibhai alisema kwamba tiketi za tamasha hiyo zitaanza kuuzwa Oktoba 25, 2023.

Bendi ya UB40 ambayo muziki wake ni mtindo wa Reggae na Pop ilianzishwa Disemba 1978 huko Birmingham Uingereza.

 

Website | + posts