Home Michezo Uasin Gishu ina uwezo kuandaa mechi za AFCON 2027, asema Bii

Uasin Gishu ina uwezo kuandaa mechi za AFCON 2027, asema Bii

0

Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii amejitokeza kimasomaso kutetea uwezo wa kaunti yake kuandaa mechi za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON mwaka 2027.

Bii amesema kuwa uwanja wa Kip Keino unaojengwa una uwezo kuselehi mashabiki 20,000 na pia miundombinu kama vile mikahawa na usalama wa kutosha kuandaa kipute hicho.

Gavana huyo alikuwa akikanusha madai ya Magavana Prof. Anyang Nyongó wa wa Kisumu na mwenzake wa Kakamega Fernandes Barasa waliodai mechi za AFCON mwaka 2027 hazipaswi kuandaliwa katika kaunti hiyo ya Uasin Gishu kutokana na hali yake duni.

Kenya imetwikwa jukumu la kushirikiana na mataifa jirani ya Tanzania na Uganda kuandaa makala ya mwaka 2027 ya fainali za AFCON.

Website | + posts