Home Habari Kuu Twitter yaweka kiwango cha jumbe ambazo kila mtumizi anaweza kuona na kusoma

Twitter yaweka kiwango cha jumbe ambazo kila mtumizi anaweza kuona na kusoma

0

Watumizi wa kitandazi cha Twitter sasa wamewekewa kiwango cha jumbe au tweets za watu wengine ambazo wanaweza kufikia na kusoma kwa siku.

Mmiliki wa mtandao huo Elon Musk alielezea kupitia mtandao huo huo kwamba watumizi ambao hawajalipia uthibitisho wa akaunti zao wanaweza tu kuona na kusoma ljumbe 1000 kwa siku, watumizi wapya 500 na waliolipia uthibitisho wanaona na kusoma jumbe 10000 kwa siku.

Kulingana na Musk wizi wa data ndio umesababisha wachukue hatua hizo za kuweka kiwango cha jumbe. Anasema watumizi wamehadaiwa na wezi wa data ambao huwaletea jumbe za kuingia upya kwenye akaunti zao wakiwa tayari wamefungua. Hata hivyo mkwasi huyo ameelezea kwamba hatua hiyo ya kuweka kiwango cha jumbe kwa kila mtumizi ni ya dharura na ya muda tu.

Alisema pia kwamba kuna watu ambao wamezoea kutumia Twitter wakati wote na anatumai hatua hiyo itawasaidia waangazie mambo mengine. “Ninafanyia ulimwengu kitu kizuri hapa.” Musk alijitetea.

Huenda Musk anazungumzia hatua ya kampuni zinazounda programu za kompyuta ambazo zinaweza kufanya kazi kama binadamu kwenye kompyuta almaarufu artificial intelligence. Kampuni hizo zinahitaji data ya kuzoesha programu hizo mawasiliano na lugha ya binadamu na mtandao kama Twitter ambao una watumizi wengi ndio unalengwa.

Twitter na kampuni nyingine zinataka zilipwe kwa data hiyo.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here