Home Michezo Tuzo za SOYA zaahirishwa hadi Machi 1 kufuatia kifo cha Kiptum

Tuzo za SOYA zaahirishwa hadi Machi 1 kufuatia kifo cha Kiptum

0

Makala ya 20 ya tuzo za kila mwaka za kuwatunuku wanaspoti bora nchini maarufu kama SOYA yataandalwia tarehe 1 mwezi ujao katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa KICC baada ya kusongezwa mbele kutoka Februari 23.

Kulingana na waandalizi wamelazmilika kuahirisha tuzo hizo, ili kutoa heshima na fursa ya kumuomboleza marehemhu Kelvin Kiptum mwanariadha ambaye alikuwa anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za marathon.

Kiptum ambaye alivunja rekodi ya dunia katika mbio za Chicago mwaka uliopita alikuwa amejumuishwa kuwania tuzo ya mwaspoti bora wa mwaka 2023 kwa wanaume pamoja na wanariadha wenza Daniel Simiu,Emmanuel Wanyonyi,mchezaji raga Patrick Odongo,na mchezaji Voliboli Simon Kipkorir.

Tuzo za SOYA ziliasisiwa mwaka 2000 na aliyekuwa bingwa mara tano wa dunia katika mbio za nyika Paul Tergat ambaye ni Rais wa kamati ya Olimpiki nchini NOCK.

Makala ya mwaka huu yatajumuisha vitengo 16 huku watakaotangazwa washindi wa vitengo mbalimbali wakipokea donge nono la pesa.

Website | + posts