Home Vipindi Tutumie sanaa kutunza mazingira, vijana waambiwa

Tutumie sanaa kutunza mazingira, vijana waambiwa

0
Photo by Jackson Mnyamwezi; KBC

Wakulima, wafanyabiashara na mashirika mbalimbali ya serikali na kibinafsi yako tayari kuonyesha bidhaa na huduma zao mbalimbali kwa umma wakati maonyesho ya kilimo na biashara ya Nairobi yaliyoanza siku ya Jumatatu jijini Nairobi yakiingia siku ya pili hii leo.

Kunao waliokuwa wakifanya gusagusa zao za mwisho za maandalizi.

Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni “kukuza kilimo na miradi ya kibiashara yenye mapato kwa ukuaji wa uchumi endelevu.”

Yanalenga kuleta pamoja wadau katika sekta ya kilimo na biashara, ikiwa ni pamoja na viwanda, biashara ndogondogo na za wastani.

Ubunifu, teknolojia za kisasa za kuboresha kilimo, huduma za kifedha na matangazo, pamoja na maonyesho ya moja kwa moja ni baadhi ya mambo ambayo watakaohudhuria watashuhudia.

Kwa Ben Wanjusi Nakitare, mkutubi mkuu kutoka makavazi ya kitaifa anasema licha ya wao kuja hapa kuonyesha huduma zao, wamefika hapa vile vile kuhamasisha umma kuhusu utunzi wa mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia sanaa.

Website | + posts