Home Taifa Tutawapiga msasa vilivyo Mawaziri wateule, aahidi Ichung’wah

Tutawapiga msasa vilivyo Mawaziri wateule, aahidi Ichung’wah

0
kra

Bunge la Kitaifa limeahidi kuwapiga msasa vilivyo Mawaziri wote 20 walioteuliwa na Rais William Ruto kuhudumu katika Baraza Jipya la Mawaziri. 

Ahadi hiyo imetolewa na kiongozi wa wengi katika bunge hilo Kimani Ichung’wah.

kra

Wanachama wa kamati ya bunge hilo inayoshughulikia uteuzi walikutana leo Alhamisi kukubaliana juu ya kanuni za kufuatwa wakati wa mchakato wa usaili.

“Kabla ya usaili wa Mawaziri wateule, Kamati ya Uteuzi iliandaa mkutano kuratibu kanuni za uidhinishaji wa watu 20 walioteuliwa kuwa Mawaziri ambao majina yao yamewasilishwa bungeni,” alisema Ichung’wah ambaye pia ni mbunge wa Kikuyu.

“Tumejitokea kuwapigia msasa vilivyo watu wote watakaofika mbele ya kamati, na kuhakikisha mchakati huo unafanywa bila chuki, upendeleo au roho mbaya.”

Rais William Ruto amewatea watu 20 kuhudumu katika Baraza Jipya la Mawaziri.

Wao ni pamoja na: 

  1. John Mbadi – Waziri wa Fedha
  2. Salim Mvurya – Waziri wa Biashara
  3. Rebecca Miano – Waziri wa Utalii
  4. Opiyo Wandayi – Waziri wa Nishati
  5. Kipchumba Murkomen – Waziri wa Masuala ya Vijana na Michezo
  6. Hassan Joho – Waziri wa Madini
  7. Dkt. Alfred Mutua – Waziri wa Leba
  8. Wycliffe Oparanya – Waziri wa Vyama vya Ushirika
  9. Justin Muturi – Waziri wa Utumishi wa Umma
  10. Stella Soi – Waziri wa Jinsia
  11. Prof. Kithure Kindiki – Waziri wa Usalama wa Kitaifa
  12. Aden Duale – Waziri wa Mazingira
  13. Debra Mlongo Barasa – Waziri wa Afya
  14. Davis Chirchir – Waziri wa Barabara na Uchukuzi
  15.  Soipan Tuya – Waziri wa Ulinzi
  16.  Eric Muga – Waziri wa Maji
  17.  Julius Migosi – Waziri wa Elimu
  18.  Alice Wahome – Waziri wa Ardhi
  19.  Dkt. Margaret Ndung’u – Waziri wa Habari na Mawasiliano
  20.  Dkt. Andrew Karanja – Waziri wa Kilimo

Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi pia anahudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje na hatahitaji kupigwa msasa kwani hakuwa miongoni mwa mawaziri waliofurushwa Baraza la Mawaziri la zamani lilipovunjwa.

Hadi kufikia sasa, ni nyadhifa mbili pekee za Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mwanasheria Mkuu ambazo hazijajazwa.