Home Michezo Tusker FC na Kakamega Homeboyz kumenyana Jumamosi kuwania kombe Mozartbet

Tusker FC na Kakamega Homeboyz kumenyana Jumamosi kuwania kombe Mozartbet

Ili kufuzu kwa fainali Tusker waliibandua Ulinzi stars bao 1 kwa bila huku Kakamega Homeboyz wakiinyuka AFC Leopards magoli 2-1 katika hatua ya semi fainali.

0

Tusker FC watachuana na Kakamega Homeboyz Jumamosi saa taisa katika uwanja wa Kasarani kuwania kwenye fainali ya kombe la Mozzartbet.

Mshindi wa fainali hiyo atatuzwa shilingi milioni 2 na tiketi ya kuwakilisha Kenya katika kombe la shirikisho Afrika msimu ujao.

Timu ya pili itaenda nyumbani na kitita cha shilingi milioni 1,nafasi ya tatu laki saba unusu na timu ya nne ituzwa shilingi nusu milioni.

Ili kufuzu kwa fainali Tusker waliibandua Ulinzi stars bao 1 kwa bila huku Kakamega Homeboyz wakiinyuka AFC Leopards magoli 2-1 katika hatua ya semi fainali.

Fainali ya Jumamosi itatanguliwa na mchuano wa kuwania nafasi ya tatu kati ya Leopards na Ulinzi Stars .

Mechi zote mbili zitarushwa mbashara kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here