Home Habari Kuu Tumekusanya sahihi zaidi ya milioni 10, wasema Azimio

Tumekusanya sahihi zaidi ya milioni 10, wasema Azimio

Haya yamefichuliwa Jumamosi na kiongozi wa muungano huo Raila Odinga kwenye kikao na wanahabari mtaani Karen.

0

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya umefichua kuwa umekusanya sahihi zaidi ya milioni 10 zinazotosha kufanya maamuzi muhimu dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza.

Haya yamefichuliwa Jumamosi na kiongozi wa muungano huo Raila Odinga kwenye kikao na wanahabari mtaani Karen.

Hata hivyo, Raila alisema wamekusanya sahihi zaidi ya milioni 10 tangu Julai 11 mwaka huu na kuwa hawatarejelea maandamano bali watachukua hatua ambayo hakuifichua.

“Vile mnavojua, tumekuwa tukikusanya sahihi kutoka kwa wananchi. Saa hii tumeshafikisha milioni kumi na zaidi, sasa imetosha gari nafahamu yale tutafanya na hizo sahihi,” alisema Raila.

Odinga alizindua shughuli ya ukusanyaji sahihi kupitia kwa mtandao mnamo Julai 11.

Ameikosoa serikali ya Kenya Kwanza kwa kufanya kinyume cha ahadi zao kwa Wakenya.

Website | + posts