Home Habari Kuu EACC yakabidhi mali ya wizi ya shilingi milioni 410 kwa kaunti ya...

EACC yakabidhi mali ya wizi ya shilingi milioni 410 kwa kaunti ya Kisumu

0

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC imekabidhi serikali ya kaunti ya Kisumu mali ya kima cha shilingi milioni 410 iliyojengwa katika ardhi iliyoporwa.

Mali hiyo inajumuisha kipande cha ardhi katika eneo la Dunga, kaunti Kisumu cha kima cha shilingi milioni 60 na jumba la ghorofa la Sunshine Villas la thamani ya shilingi milioni 350 lililojengwa katika kipande hicho cha ardhi.

Menaja wa tume ya EACC eneo la magharibi Abraham Kemboi amekabidhi mali hiyo leo Jumatatu kwa serikali ya kaunti ya Kisumu ikiwakilishwa na meneja wa jiji hilo Abala Wanga.

Website | + posts