Kampuni ya Tullow Oil imeelezea matumaini yake kuhusu mafuta ghafi yaliyochimbwa eneo la Turkana.
Afisa Mkuu Mtendaji wa kamouni ya Tullow Oil Plc Rahul Dhir amesema kuwa kampuni hiyo tayari imeanza mazungumzo na waekezaji wa kimkakati.
Washirika wa awali, kampuni ya TotalEnergies na Africa Oil, walitangaza kujiondoa mwezi Mei mwaka huu kutoka maeneo ya Lokichar Kusini, kaunti ya Turkana ambapo uchimbji wa mafuta ghafi haujaanza.
“Tunafurahia sio tu kuwa nchini Kenya lakini pia kuwa katika eneo hilo ambapo tumepewa mulaka mzuri kutoka kwa uongozi wa kaunti na jamii. Tumeshuhudia mabadiliko makubwa tangu ujio wa uongozi wa serikali mpya, ”alisema Dhir.
Usimamizi wa Tullow Oil umeitaka serikali kuharakisha mchakato wa uzalishaji mafuta katika eneo hilo.