Home Habari Kuu Tshisekedi anusia muhula wa pili akiongoza kwa asilimia 76 ya kura DRC

Tshisekedi anusia muhula wa pili akiongoza kwa asilimia 76 ya kura DRC

0

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Félix Tshisekedi amejihakikishia muhula wa pili afisini akiongoza kwa asilimia 76 ya kura zote za uchaguzi mkuu wa Disemba 20 na 21 uliofanywa nchini humo. 

Kulingana na tume ya Uchaguzi, kati ya kura milioni 12.5 zilizohesabiwa, Tshisekedi aliye na umri wa miaka 60 amezoa kura milioni 9.5.

Mfanyabiashara na Gavana wa zamani Moïse Katumbi ni wa pili kwa asilimia 16.5 huku Martin Fayulu akiwa wa tatu kwa asilimia 4.4.

Vyombo vya habari nchini humo tayari vimemtangaza Tshisekedi kuwa mshindi ingawa tume ya uchaguzi ina hadi Disemba 31 kutangaza matokeo.