Tume ya kuwaajiri walimu TSC imelalmikia utelekazaji katika kaunti ya Bungoma kufuatia wanafunzi 11,601, waliokalia mtihani wa KCPE mwaka 2023 waliokosa kujiunga na kidato cha kwanza.
Maafisa wa Serikali ya katika kaunti ya Bungoma wameanza shughuli ya kuwatafuta wanafunzi wote ambao hawajiripoti kidato cha kwanza na kuwapeleka shuleni.
Kulingana na Mkurugenzi wa TSC kaunti ya Bungoma, Machifu,viongozi wa nyumba kumi na maafisa wa serikali wanaendeleza msako wa kuwatafuta na kuwapeleka shuleni wanafunzi ambao wangali nyumbani katika kaunti hiyo.