Home Kimataifa Trump kizimbani katika kesi ya ulaghai dhidi ya familia yake

Trump kizimbani katika kesi ya ulaghai dhidi ya familia yake

0

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amefika kwenye mahakama moja huko Manhattan, kutoa ushahidi kwenye keshi ya ulaghai huko New York dhidi ya familia yake.

Uchunguzi huo unaongozwa na wakili wa jiji la New York Letitia James na ulifahamika mwaka 2020, wakati mwanawe Trump kwa jina Eric Trump alishindwa kupinga kisheria agizo la kumtaka afike mahakamani.

Miaka miwili baadaye afisi ya wakili James ikaweka kesi ya dola milioni 250 mahakamani, ambapo analaumu Trump, shirika la Trump na wafanyakazi wakuu wa shirika hilo akiwemo Eric na Donald Trump Jr kwa mpango wa mwaka mzima wa ulaghai.

Wote hao wamekuwa wakikana makosa hayo huku Trump akisema kwamba wakili James amemotishwa kisiasa kumfuatilia.

Trump alifika kwenye mahakama hiyo muda mfupi kabla ya saa nne asubuhi ambapo alihutubu kidogo kabla ya kuingia ndani ya jengo la mahakama.

Kwenye hotuba hiyo fupi, Trump alisema kwamba anakabiliwa na mahasimu wa kisiasa na ni suala la kuhuzunisha kwa nchi ya Marekani.

Awali wakili James alibashiri kwamba angetukanwa na Trump lakini akasema hatishiki kwani mwisho wa siku, kitu muhimu ni ukweli.

Jaji hakukubalia wanahabari ndani ya mahaka ilivyotarajiwa awali kumaanisha kwamba kesi hiyo haitapeperushwa mubashara.

Trump anasemekana kufaidika na mpango wa ulaghai wa kuashiria kwamba utajiri wa familia yake ni wa kiwango cha juu kuliko kiwango halisi.

Anasemekana pia kuongeza thamani ya mali yake kwa lengo la kupata mkopo wa kiwango kikubwa na masharti bora ya bima.

Jaji anayesikiliza kesi hiyo, tayari amempata Trump, wanawe waili wa kiume na kampuni yao na makosa ya ulaghai.