Home Kimataifa Trump ashtakiwa kwa mara ya nne

Trump ashtakiwa kwa mara ya nne

0

Aliyekuwa rais wa marekani Donald Trump na rafikize 18 wameshtakiwa katika jimbo la Georgia nchini humo kwa kupanga njama ya kupindua ushinde wake kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.

Kesi hiyo ya Jumatatu Agosti 14, 2023 ndiyo kesi ya nne dhidi ya Trump na ya pili mwezi huu inayohusiana na uchaguzi wa urais mwaka 2020.

Mkuu wa wafanyakazi katika ikulu wakati Trump alikuwa rais Mark Meadows na mawakili Rudy Giuliani na John Eastman ni kati ya washtakiwa katika kesi hiyo.

Mashtaka hayo yaliyoibuliwa na mwanasheria wa wilaya ya Fulton, Fani Willis, yanatokana na uchunguzi ulioanzishwa punde baada ya kutolewa kwa mazungumzo ya simu yaliyonakiliwa kati ya Trump na Brad Raffensperger msimamizi wa jimbo la Georgia Januari 2, 2021.

Kwenye mazungumzo hayo ya simu Trump anasikika akimwelekeza Raffensperger afanye awezalo apate kura 11,780, idadi ambayo ingemwezesha kushinda Joe Biden.

Trump wa chama cha Republican, ametaja mazungumzo hayo ya simu na Raffensperger kama yanayofaa huku akitaja kesi dhidi yake kuwa inayochochewa na siasa.

Wakili Jack Smith amekuwa akiongoza uchunguzi dhidhi ya Trump, na amepata ana makosa. Makosa ya kwanza yalionekana mwezi juni wakati ambapo Trump alishtakiwa kwa kutolinda ifaavyo stakabadhi muhimu na za siri nyumbani kwake huko Florida.

Kosa jingine linatokana na hatua ya rais huyo wa zamani ya kutaka video za kamera za ulinzi katika makazi yake ya Mar-a-Lago zifutwe wakati wapelelezi wa FBI walimzuru mwezi Juni mwaka 2022 kuchukua stakabadhi muhimu ambazo alitoka nazo ikulu ya White House.

Anatuhumiwa pia kwa kukatalia stakabadhi fulani yenye umuhimu mkubwa na ambayo alikuwa akionyesha wageni wake.

Kwa jumla makosa dhidi ya Trump ni takribani 40 huku kila kosa likiwa na adhabu ya miaka kama 20 gerezani kulingana na sheria.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here