Home Habari Kuu Trump afungiwa nje ya kinyang’anyiro cha kurejea White House

Trump afungiwa nje ya kinyang’anyiro cha kurejea White House

0

Mwaniaji Urais nchini Marekani kwa chama cha Republican Donald Trump, amepatwa na pigo kubwa, baada ya mhakama ya upeo katika jimbo la Colorado kuamua kuwa hafai kuwa kwenye debe.

Katika uamuzi huo mahakama imeamrisha katibu wa ikulu kuondoa jina la Trump kwenye nchujo wa chama cha Republican.

Ni mara ya kwanza na tukio la kihistoria kwa mahakama ya upeo kutoa uamuzi wa kumfungia nje mwaniaji Urais kutokana na kuhisika kwake kwa vita dhidi ya raia katika shambulizi la Januari 6 mwaka 2021 mjini Newyork.

Trump ambaye alikuwa Rais kwa muhula mmoja, alifunguwa nje ya kurejea katika ikulu ya White House, kwa kutumia kipengee cha 3 na 4 cha sheria ya taifa hilo kilichofanyiwa marekebisho.

Hii ina maana kuwa Republican watalazimika kumteua mwaniaji mwingine atakayekabiliana na Rais Joe Bidden wa chama cha Democratic, katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Website | + posts