Home Burudani Torry Lanez ahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani

Torry Lanez ahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani

0

Mwanamuziki wa mtindo wa rap kutoka Canada Tory Lanez alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani Jumanne kutokana na makosa ya kumpiga risasi mguuni mwanamuziki Megan Thee Stallion.

Hilo lilitokea yapata miaka mitatu iliyopita wakati wawili hao walikuwa wanaondoka kwenye sherehe ya nyumbani ambayo walikuwa wamehudhuria Julai 2020, huko Hollywood Hills. Ugomvi ulizuka kati yao walipojibizana kuhusu uhusiano wao na kazi zao ndiposa Lanez akamfyatulia Megan risasi mguuni.

Mawakili wa Megan walikuwa wameomba Lanez ahukumiwe kifungo cha miaka 13 gerezani.

Lanez amekuwa gerezani tangu Disemba 2022 wakati mahakama ilimpata na hatia katika makosa matatu yanayohusiana na tukio hilo ambayo ni kushambulia kwa bunduki, kubeba kwenye gari bunduki ambayo haijasajiliwa ikiwa na risasi na kufyatua risasi bila kujali.

Mawakili wa Lanez walikuwa wanataka kifungo chake kiwe cha nje lakini viongozi wa mashtaka walipinga ombi hilo wakisema mshtakiwa ana utepetevu wa kiwango cha juu kulingana na kitendo cha siku hiyo cha kumfyatulia mwenzake ambaye hakuwa na silaha risasi na mwenzake hakuwa amemchokoza.

Viongozi wa mashtaka walisema Lanez anastahili kifungo cha muda mrefu gerezani.

Lanez, ambaye jina lake halisi ni Daystar Peterson, amekuwa akikanusha mashtaka yoye dhidi yake kwenye kesi hiyo. Jaji wa mahakama ya jimbo la Los Angeles David Herriford alisema mahakamani kwamba alipokea barua 70 kutoka kwa watu ambao walikuwa wanaonyesha kwamba wanamuunga mkono Lanez.

Megan kwenye taarifa yake kuhusu athari alizopata kutokana na shambulio la Lanez iliyosomwa mahakamani alisema Lanez alichukulia kiwewe na maumivu yake kama mzaha ilhali angepoteza maisha siku hiyo.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here