Home Kimataifa Tom Mshindi ateuliwa mwenyekiti wa bodi ya shirika la KBC

Tom Mshindi ateuliwa mwenyekiti wa bodi ya shirika la KBC

Rais Ruto alifutilia mbali uteuzi wa mhandisi Benjamin Maingi kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo.

0
Tom Mshindi.
kra

Rais William Ruto amemteua Tom Mshindi, kuwa mwenyekiti wa bodi ya usimamizi ya shirika la utangazaji nchini KBC, kwa kipindi ya miaka mitatu.

Kupitia kwa gazeti rasmi la serikali siku ya Ijumaa tarehe 19 mwezi Januari mwaka 2024, Rais Ruto alifutilia mbali uteuzi wa mhandisi Benjamin Maingi kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo.

kra

“Kulingana na mamlaka niliyonayo kupitia sehemu ya 7 (3)  ya sheria za shirika la utangazaji nchini…….namteua Tom Mshindi Nyamancha kuwa mwenyekiti wa bodi ya shirika la utangazaji nchini KBC kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia tarehe 19 mwezi Januari mwaka 2024,” ilisoma arifa hilo.

Tom Mshindi alihitimu kutoka chuo kikuu cha Nairobi, ambako alisomea uanahabari, kabla ya kufanya kazi katika vituo mbali mbali vya habari hapa nchini.

Mshindi pia aliwahi kuwa mhariri katika shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF, Jijini New York Marekani.

Website | + posts