Bingwa wa dunia katika mbio za mita 110 Tobi Amusan kutoka Nigeria atakosa kutetea taji ya dunia mwezi ujao mjini Budapest nchini Hungary baada ya kupigwa marufuku na kitengo cha maadili ya wanariadha, AIU kwa makosa matatu ya kukwepa vipimo vya ulaji muku.
Amusan aliye na umri wa miaka 26 alishinda dhahabu ya dunia mwaka jana katika mashindano ya dunia huku akivunja rekodi ya mita 110 kuruka viunzi.
Endapo makosa hayo ya kukwepa vipimo yatathibitishwa baada ya uchunguzi, Amusan anakabiliwa na hatari kufuingiwa kushiriki mashindanoni kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.