Home Michezo Timu zitakazocheza nusu fainali ya mataji ya CAF kubainiki

Timu zitakazocheza nusu fainali ya mataji ya CAF kubainiki

0

Timu zitakazocheza nusu fainali ya mataji ya Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho la soka Afrika zitabainika  mwishoni mwa juma hili baada ya marudio ya kwota fainali.

Katika Ligi ya Mabingwa,washindi wa mwaka jana Al Ahly ya Misri ukipenda Red Devils watawaalika miamba wa Tanzania bara Simba Sports Club Ijumaa kuanzia saa tatu usiku,wenyeji wakiongoza bao 1 kwa bila kutokana na duru ya kwanza.

Mchuano mwingine wa robo fainali utashuhudia Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wakiwakaribisha mabingwa wa Tanzania Yanga Ijumaa kuanzia saa tano usiku.

Jumamosi Petro Atletico ya Angola itawaalika TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo siku ya Jumamosi baada ya sare tasa katika mkumbo wa kwanza huku Esperance ya Tunisia wakiwa ziarani  Ivory coast kukabiliana na Asec Mimosas.

Katika kombe la Shirikisho Dreams ya Ghana inayoongoza 2-1 itawaalika Stade Malien ya Mali Jumapili huku Zamalek wanaongoza pia 2-1 dhidi ya wenzao Future FC wakiwa nyumbani.

Jumatatu Rivers United ya Nigeria watakuwa ziarani mjini Algiers dhidi USM Alger nao Berkane ya Moroko waialike Abu Salim ya Libya timu zote zikitoka sare tasa katika duru ya kwanza.

Website | + posts