Home Michezo Timu za soka za Kenya zawasili China kwa mashindano ya dunia

Timu za soka za Kenya zawasili China kwa mashindano ya dunia

0

Vikosi vya timu ya taifa vya soka kwa akina dada na wavulana vitakavyo shiriki mashindano ya kimataifa baina ya shule za upili mjini Dalian nchini Uchina, vimewasili nchini humo.

Timu ya wavulana ni kama ifuatavyo: Joseph Omuse na Abdulkadir Dahir (St. Antony-Kitale), Austin Odongo (Ebwali), Joseph Owino (Kisumu Day), Nicholas Odhiambo, Elisha Nalianya na Idris (Menengai High), Ostosyi na Aroko (Highway High NRB), Robert Mutie (Makueni), Osoro (Christ the King), Ndungu Joseph (Laiser Hill), Hirald na Malcolm (Musingu).

Kikosi hiki kitaongozwa ma mwalimu/mkufunzi Peter Mayoyo wa St. Antony Kitale.

Kwa upande wa akina dada, orodha ni ifuatayo: Felisters atieno ( magunga), Joy Marvelous(Ogande-Homabay), Precious Zawadi(Trinity Mission-Nakuru), Mercy Akoth (Nyakach), Sheila Kemunto, Elizabeth Mideva na Dalphine Ayesa (ABN-Kakamega), Sunira Were(Moi-Eldoret), Vidah Okeyo, Christine Adhiambo na Clotildah Auma (Butere), Fatuma Wanja (st. Alfred-Machakos), Yvone Kangashi (Dagoretti Mixed), Mitchelle Waithera (St.Alfred-Alara), Faith Baraza na Ruth Achieng ( Nasokol-West Pokot).

Kikosi hiki kinaongozwa na kocha wa shule ya upili ya wasichana ya Arcbishop Njenga-Kakamega Fred Serenge.

Kipute hicho kitango’a nanga’a tarehe 17 hadi 27 mwezi huu siku chache baada ya Kenya kuandaa riadha ya mashindano hayo.