Home Michezo Timu ya Kenya ya voliboli yaishinda Uganda kwenye michezo ya wabunge

Timu ya Kenya ya voliboli yaishinda Uganda kwenye michezo ya wabunge

0

Timu ya Kenya ya mchezo wa voliboli ya wanaume ilionyesha ujuzi wake na kutawala wapinzani wao Uganda na kuwashinda alama 3 kwa 1 kwenye michezo inayoendelea ya wabunge Afrika Mashariki jijini Kigali nchini Rwanda.

Mashabiki waliokuwa wakitizama mashindano hayo katika uwanja wa Ecole Notre Dame Des Anges walisisimka baada ya wabunge wa Kenya chini ya nahodha Dan Wanyama mbunge wa Webuye Magharibi kuibuka washindi.

Ushirikiano mwema kati ya wachezaji wa Kenya uliwapa ushindi wa seti za alama 25-17,22-25,25-20,25-23 dhidi ya Uganda.

Wachezaji wengine kwenye timu hiyo ni pamoja na maseneta Jackson Mandago na Seki Lenku, wabunge Victor Koech, Maina Mathenge, Brighton Yegon, Alfred Mutai na Paul Nzengu.

Huo ndio ulikuwa mchuano wa kwanza wa timu ya Kenya na sasa ina matumaini ya kuendeleza matokeo bora katika mechi zilizosalia.

Website | + posts