Home Habari Kuu Timu ya Kenya Kwanza inapaswa kuvunjwa, asema mbunge wa Lugari

Timu ya Kenya Kwanza inapaswa kuvunjwa, asema mbunge wa Lugari

0

Mbunge wa Lugari Nabii Nabwera sasa anamtaka Rais William Ruto kuvunja timu ya upande wa Kenya Kwanza iliyobuniwa ili kushiriki mazungumzo na muungano wa Azimio.

Timu ya Kenya Kwanza inajumuisha kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kimani Ichung’wah, Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot, Gavana wa Embu Cecily Mbarire, Mwakilishi wa Wanawake katika kaunti ya Bungoma Catherine Wambilianga na mbunge wa EALA Hassan Omar.

Hata hivyo, Nabwera anadai timu hiyo haina maadili na huenda isiafikie matokea chanya.

Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi ya Tekoa katika eneo bunge lake la Lugari.

Kauli zake zikiwadia wakati Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa ametoa wito kwa serikali na upinzani kutoa kipaumbele kwa maslahi ya Wakenya wakati wa mazungumzo kati yao.

Akizungumza katika eneo buunge la Malava mapema leo Jumatatu, Barasa alisisitiza haja ya kuwepo ajenda itakayolinufaisha taifa lote bila dhamira yoyote fiche.

Kadhalika alisisitiza umuhimu wa uwazi wakati wa mazungumzo hayo na kutoa wito kwa viongozi kuweka kando tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa ya Wakenya wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here