Home Michezo Timu ya Kenya kwa mbio za barabara duniani kuondoka Jumatano

Timu ya Kenya kwa mbio za barabara duniani kuondoka Jumatano

Kenya itawakilishwa na wanariadha 21 wanaume 10 na wanawake 11,wengi wao wakiwa wale walioshiriki mashindano ya dunia mjini Budapest Hungary mwezi uliopita.

0

Kikosi cha Kenya kwa makala ya mwaka huu ya mashindano ya mbio za barabara duniani kitaondoka nchini Septemba 27 kuelekea mjini Riga, nchini Latvia.

Timu hiyo imekuwa kwenye mazoezi kujiandaa kwa mashindano hayo.

Mashindano ya mwaka huu yataandaliwa kati ya Septemba 30 hadi Oktoba mosi.

Kenya itawakilishwa na wanariadha 21, wanaume 10 na wanawake 11, wengi wao wakiwa wale walioshiriki mashindano ya dunia mjini Budapest nchini Hungary mwezi uliopita.

Washiriki wa mbio za umbali wa maili moja ni:- Reynold Kipkorir Cheruiyot, Nelly Chepchirchir, Beatrice Chepkoech na bingwa mara tatu wa dunia katika mita 1500 Faith Kipyegon.

Mbio za nusu marathon zitawashirikisha:- Daniel Simiu, Charles Kipkurui, Samwel Nyamai, Sabastian Kimaru, Benard Kibet, Janeth Chepngetich, bingwa mtetezi Peres Jepchirchir, Irine Jepchumba, Margaret Chelimo na Catherine Relin.

Katika mbio za kilomita tano, wanariadha watakaotimka ni:- Cornelius Kemboi, Nicholas Kipkorir, Stanley Waithaka, bingwa wa dunia wa mbio za nyika Beatrice Chebet, Caroline Nyaga na Lilian Kasait.

Website | + posts