Home Habari Kuu Tetemeko kubwa la ardhi latokea kusini magharibi mwa Japani

Tetemeko kubwa la ardhi latokea kusini magharibi mwa Japani

0
kra

Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.1 kwenye kipimo cha Richter limetokea kusini magharibi mwa Japani.  

Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini humo imetoa tahadhari ya kutokea kwa tsunami katika mikoa ya Miyazaki, Kochi, Oita, Kagoshima na Ehime.

kra

“Kama upo katika maeneo yaliyoathiriwa, kaa mbali na maeneo ya pwani na kwenye mito inayoweza kufurika. Endelea kuhama hadi ushauri wote uondolewe,” unasema ushauri uliotolewa kwa wananchi katika maeneo yaliyoathiriwa.

“Huenda kukawa na mabadiliko kadhaa kwa kiwango cha bahari, lakini hakuna tishio la kutokea kwa uharibifu wa tsunami. Mawimbi yanaweza yakawa makubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa.”

Mamlaka bado zinafuatilia hali ya mambo na kuutarifu umma mara kwa mara juu ya hatua za kuchukua kufuatia kutokea kwa tetemeko hilo.

 

 

Website | + posts